Monday, August 27, 2007

UMEPONA?

Jamaa ni miongoni wa waliopewa shavu na prezda we2 wa motco msela ni waziri wa elimu,juzi nilimtembelea hosp alikuwa anasumbuliwa na malaria sasa leo nimekanyaga kwa ofis nikamkuta nikampa hiyo..kaka umepona au umemiss pc

NIMEWAKUBALI MANISPAAA....!!!

Ni nyakati za mchana nilipotembelea town niliwakuta wafanyakazi wa manispaa ya mji kasoro bahari wakiwajibika ktk kutoa mabaki ya tope yaliyomo ktk mitaro kuzunguka stend ndogo ya mkoa.Hongera sana manispaa kwani tahadhari ni bora kuliko kusubiri

MDAU KANITUMIA

Ahsante sana mdau kwa kunitumia hiyo

MAJADILIANO.....?

Wanachama wa ccm mg vijijini wakijadiliana mawili matatu kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa waakilishi wao mkoa

KIJIWE KINAPOKUWA KIGUMU...!!

Hii nayo niliivyatua nikiwa ktk daladala..inaonekana jpili ni cku nzito sana kwa taxi hizi.....

KUTOKA DIRISHA LA HIACE

Hata barclays inapatikana mji kasoro bahari..hii snap nilinyaka nikiwa ndani ya daladala nilikua najaribu kutenda kama atendavyo mdau wangu mkuu cpwaaaaa....!

SOKO KUU LA MJI KASORO BAHARI

SIO KWAMBA AMEGRADUATE


Jamaa nilimnyaka na mashine yangu d410 maeneo ya uchaguzi wa ccm wajumbe halmashauri kuu ya ccm mkoa.Nilifikiri mkuu alikua ametoka kula nondo yake kumbe alikuwa ametoka ktk uchaguzi safi sana kidumu chama cha mapinduzi.......!!!!!

MAXIMO UMEWAONA HAWA?



Ni miongoni mwa mambo ya vituli hawa vijana kutoka kitaaani wako hapa collage mida ya jioni katika kiwanja cha vituli kwa kujifua hii ni kutokana na uhaba wa viwanja vya michezo huko kitaani kwao..kocha maximo anahitajika kutembelea hapa mana madogo wanakamua kisawaswa kama brasil vile

IMESAIDIA MKUU...!

Ni dk30 kabla ya lokoo ya jmosi watu walikuwa wamefurika kutokana na kauli ya mkuu..sasa jamani kumbe inawezekana sasa iweje mpaka tusubiri?

MENEJA UPO?


Raisi aliliona hili ndo mana akateua msimamizi mkuu wa eneo hili..sasa iweje mazingira ya eneo hili yawe kiivyo?Mi naomba watumiaji tushirikiane kufanikisha hili ili jamaa asipigwe chin

HUU NI UWANJA NASIO KAMBA YA KUANIKIA NGUO


Nafikiri wale wadau flani watakua wamenipata kwa dhati kabisa hii sehemu sio ya kuanika viwalo kwa haiba ya watu wa hapa hairuhusu kaweka vitu kama hv hadharani...