Monday, August 20, 2007

MWALIMU UBUNIFU...


Ka mjengo hapo juu nilishiriki ktk kudesign na tenda niliramba from foundation hadi finishing...sasa sio class tu hata akili ya kaz nayo inahitajika wadau..

NAKUTAFUTA POPOTE ULIPO...!!!

MITAA YA USWAZI

Wadau hapo ndio maskaani kwa bi mkubwa..kuna m2 alidai eti mi mtoto wa mboga saba sasa umepaona nilipotoka mtoto wa mkulima halisi..?

MODAL...!!!!

Jamani hiko kipaji nimekivumbua mitaa ya home inshort huyo dogo anatisha kwa uelewa pongezi kwa check bob wangu kazi nzuri uliifanya muendeleze bint huyo mana ndio condoleza rice we2

BEEF HUANZIA UTOTONI...

Vijana niliwafuma ktk kibaraza cha home wkigombania kitenes palikua hapatoshi mshkaji yeye alitumia nguvu kwa kuwa mwenzake ni dogo but dogo nae hakukubali alipigana mpaka kikaeleweka..wazazi tuwe makini tunapowaruhusu watoto wenye rika linalokaribiana wanapokutana.

SIO LECTURE=ZE COMEDY

Hao ni wanajamuhuri wakifuatilia kwa umakini likipindi la ze comedy na sio lecture..niliibamba last thursday..ila naona kaluninga hakakidhi mahitaji kwani mshkaji wa nyuma hapo alikua analalama kuwa anapunjika..

WELCOME DIP 1

Ndani ya Fr.FRANKEN mkuu wa chuo akiwakaribisha mwaka wa kwanza na kufunga semina yao iliyoendeshwa kwa cku 3 juu ya kuelewa taratibu na kanuni za chuo..Jamaani 1yr semina itakuwa imeeleweka na sheria zitafuatwa..karibuni chuoni.

ILIGO CONNECTION

Jama jama mi simo nimeifuma maeneo lakini hii kidogo inausalamaaa kuna zile za denja denja jamani tutakuja kuwaka kama vp tuombe watuwekee kila room mana kuzuia ni ngumu..

HAYA SASA NIMEWALETE MSINIULIZE TENA..!!!!

UCHAFUZI WA MAZINGIRA

SIO WAKATI WA STORY.....

Jamaa hawa ni wa masomo flani yanayoongoza kwa ubishi..huu ulikua wakati wa fatick (wadau wa maeneo wamenielewa)lakini jamaa waliendelea na michapo kama uwaonavyo..oya kama mnanipata jirekebisheni sio uungwana

VITULI NOMA....!

Mpaka sasa hakuna dom iliyovunja record ktk kuaandaa party ya kukaribisha mwaka wa kwanza..ahadi ni deni niliwaahidi na nimetimiza..hapo jamaa naona full shangwe

KIBAKA....


Jamaa nilimfuma mitaa ya samora raia walikuwa wameshamporomoshe kichapo baada ya kushindwa kunyakua cm ya mzalendo..inasemekana ni kawaida ya vibaka kuwepo mitaa hiyo na wamewavumilia but raia wamechoka na katabia hicho